Mjumbe wa kamati tendaji ya Timu ya Stand United 'Chama la Wana' Geofrey Rugalema Tibakyenda  maarufu 'Tiba' amejiuzulu nafasi yake na kubaki kuwa mwanachama wa timu hiyo baada ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati tendaji ya Timu ya Polisi Tanzania 'Tanzania Police FC' inayoshiriki  Ligi daraja la kwanza ngazi ya taifa.
Tibakyenda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumamosi September 1,2018,Tibakyenda amewashukuru wanachama na mashabiki wa Stand United kwa kipindi chote alichotumikia timu hiyo katika kuipa mafanikio Stand United.

"Kama kuna mapungufu niliyokuwa nayo kama binadamu kuwakwaza viongozi wa kamati tendaji,wanachama na mashabiki ilikuwa ni kutaka kufanikisha ili Stand United kupata mafanikio,hivyo kama mwanadamu,nawaomba radhi nilipowakwaza na nilipowakosea naomba mnisamehe na nashukuru kwa ushirikiano wenu,tutazidi kushikirikiana nakupeana mawazo,karibuni mniunge mkono katika kuanza kazi yangu timu ya Tanzania Police FC",ameeleza Tibakyenda.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share To:

Anonymous

Post A Comment: