Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Tanzania, Afande Sele amesema kuwa kwa upande wa vyama vya upinzani ni Professor Jay pekee ndiye Mbunge anayeonekana kufanya kazi kwa bidii huku akimtolewa mfano Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuwa anaendekeza siasa chafu za matusi jukwaani.

Afande Sele amefunguka hayo kupitia mahojiano yake na Bongo5, ambapo amedai kuwa kauli ya Sugu kuwa mama yake amefariki kutokana na tukio la yeye kufungwa jela hilo ni kosa lake kwani alimtukana mkuu wa nchi, Rais Magufuli jukwaani jambo ambalo ni kosa kisheria.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: