Wachezaji wa Taekwondo Polisi Arusha wakimuonesha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'anzi moja kati ya show ya Mchezo huo.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akijaribu moja kati ya vifaa vya mazoezi vilivyo katika GYM ya Polisi Arusha. Kushoto kwake ni Kocha wa Timu hiyo Shija Makoye
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akisisitiza jambo wakati akiongea na Wachezaji hao.

Na Gasto Kwirini wa Polisi Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi leo ametembelea mazoezi ya Timu  ya Taekwondo ya Polisi Mkoa wa Arusha yanayofanyika kila siku iioni katika Dojo lilipo Kambi ya Polisi New Line Arusha. 

Alipata fursa ya kuona sehemu ya Mazoezi (Gym), Onesho (Show) ya Taekwondo pamoja na changamoto zilizopo katika Timu hiyo. Aidha amewapongeza wachezaji wa timu hiyo walioshiriki katika Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (EAPCCO) yaliyofanyika  Mkoani Dar es Salaam na kupata Medali mbili ya Shaba na Fedha. 

‘‘Leo nimehamasika kuungana na mazoezi haya hasa kwa kuzingatia yanatija katika kazi yetu, Kwa sababu lengo la mchezo huu ni kujenga ukakamavu na kujilinda binafsi. Kuanzia wiki ijayo nitajumuika nanyi, mwisho wa siku na mimi nivae mikanda kama yenu’’. Amesema Kamanda Ng’anzi.

Pamoja na mambo mengine amehaidi kuzifanyia kazi changamoto walizo nazo hasa la vifaa na muda wa Mazoezi kuingiliana na Ratiba za kazi. Alisema atakaa na viongozi  wenzake kuona jinsi ya kutatua changamoto hizo.

Awali akitoa historia fupi ya Timu, Kocha wa Timu hiyo Shija Makoye alisema timu hiyo inahusisha jumla ya wachezaji kumi na tano (15) ambapo wanapata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali za kujijengea ukakamavu na uwezo binafsi wa kujilinda pindi wanapokabiliana na Adui. Pia  alimweleza changamoto mbalimbali ambazo timu hiyo inakumbana nazo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: