Kamati ya Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi ya Wilaya ya Nyamagana chini ya mwenyekiti wake Mayor wa halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhe. James Bwire, wamepata fursa ya kuagana na aliyekuwa katibu wa CCM Wilaya Ndg. Clemence Mkondya ambaye hivi  sasa ni Kaimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza, kadharika kumkaribisha Ndg  Salum .A. Kalli ambaye amehamia Nyamagana kutokea Ubungo.

Akiwaaga kamati ya Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Clemence Mkondya kaimu katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza amepata fursa yakutoa nasaha na kuwapongeza kwa ushirikiano alioupata muda Wote wa utendaji wake Nyamagana. "Nawapongeza kwa umoja na mshikamano mlionipatia kipindi chote cha uongozi wangu Nyamagana nawasihi dhamira hiyo njema iendelee kwa katibu mgeni Kalli ambaye sio mgeni kwa kazi, kwani mbali ya kuwa katibu wa CCM ngazi ya wilaya kwa wilaya mbalimbali lakini pia amewahi kuwa mwenezi wa Chama" Ndg Mkondya amesema.

Akifungua kikao hicho Mayor wa halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhe. James Bwire amesema madiwani wa Chama Cha Mapinduzi wamekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi mapana ya wananchi, kujenga hoja zenye mashiko, kuonesha umoja na mshikamano thabiti katika kuisimamia serikali kupitia halmashauri ya Jiji la Mwanza kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.

Ndg. kalli amesema miongoni mwa kazi zilizomleta Nyamagana mbali na kuwa mtenda mkuu kadharika anawajibika kuisaidia CCM ishike dola pamoja na kuisimamia serikali itekeleze Ilani ya Uchaguzi. "Madiwani wanaotokana na CCM ni watu mhimu sana, na wasihi kupitia vikao vya mabaza ya kata kumkatoe mrejesho kwa wananchi utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2015-2020. Muwe chachu kwa wenyeviti wa serikali za mitaa watoe mrejesho nao, hii ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 145/146.

Ndg. Kalli amemalizia kwa kuwaomba Madiwani kuondoa tofauti  za uchaguzi ambazo zinaweza kuleta matabaka na mipasuko isiyo na tija. Amewasihi wazidi kudumisha umoja, mshikamano na upendo kwa maslahi mapana ya Chama Cha Mapinduzi. "Ninawapongeza kwa kazi kuwa ya kuwaletea wananchi maendeleo mnayoifanya, imeonekana dhahiri katika mbio za Mwenge wa Uhuru, ninawaahidi mshikamano wa kipindi chote cha uongozi wake.  Ndg Kalli amesema.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi waandamizi wa Chama  Cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana chini ya Mwenyekiti Ndg. Zebedayo pamoja na Madiwani 22 wa CCM.

Imetolewa na
Idara ya Siasa na Uenezi
Wilaya ya Nyamagana
Share To:

msumbanews

Post A Comment: