Diwani wa kata ya Nkoanekoli katika Halmashauri ya Meru wilayani Arumeru kupitia (Chadema), Ndg. Wilson Nanyaro  ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na chama a Mapinduzi CCM kwa maelezo kwamba anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Nanyaro ni diwani wa kumi na moja katika Halmashauri ya Meru kujiuzulu kwa kwa kipindi hiki  kwa kumuunga mkono Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Ndg. Emanuel Mkongo amethibitisha leo (September 27 ) kupata taarifa za kujiuzulu kwa Nanyaro.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: