Umoja wa Vijana wa CCM unapenda kuujulisha umma wa Watanzania na wanachama wote kwa ujumla kuwa kikao cha Baraza kuu la UVCCM Taifa kilichokutana jana tarehe 31 Agosti, 2018 Jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Kheri Denice James (MCC) kilifanya Uchaguzi ili kuwapata wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa ambapo wafuatao walichaguliwa:-
Tanzania Bara:-
1.Ndg. Saitoti Zelothe Steven
2. Ndg. Joanfaith John Kataraiya
Tanzania Zanzibar
1.Ndg. Abdulghafar Idrissa Juma
2.Ndg. Mariam Ally Juma
Aidha kilipokea na kuwathibitisha Wakuu wa Idara Tano za Umoja wa Vijana wa CCM Taifa kama ifuatavyo:-
1.Ndg. Peter Kasera-Katibu wa Idara ya Organaizesheni, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
2.Ndg. Lusekelo Nelson-Katibu wa Idara ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha
3.Ndg. Kamana Juma Simba-Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu.
4.Ndg. Hassan Bomboko
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi.
5.Ndg.Mohamed Abdalla
Katibu wa Idara ya Usalama na Maadili.
Pamoja na mambo mengine, Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa liliazimia yafuatayo:-
1.Pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuendelea kuwaamini Vijana katika Serikali zao na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mafanikio makubwa.
2.Pongezi kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kwa kuaminiwa na kuteuliwa na NEC kushika nafasi hiyo, pamoja na utendaji unaokirejesha Chama chetu katika misingi ya kuasisiwa kwake na maelekezo yake kwenda kutekelezwa kuanzia ngazi ya Tawi.
3.Hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa kupokelewa kama maelekezo kwa Jumuiya yetu, na kufanyiwa utekelezaji kuanzia ngazi ya Tawi.
4.Kupitisha Mpango Mkakati wa Jumuiya unalenga Kujitegemea Kiuchumi na kuimarisha Jumuiya nchi nzima ili kwenda sambamba na dhana ya Siasa ni Uchumi.
5.Tunaitaka Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa Vijanawenzetu waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi kama vile Bajaji, Bodaboda, wajasiriamali, wachimbaji wadogo, wavuvi,wapagazi, wakulima, wafanyabiashara wadogo, wasanii, MamaLishe n.k. pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa Vijana walioajiriwa viwandani, migodini n.k.
6. Kuitaka Serikali kuweka mazingira rafiki kwa vijana wenzetu wanaohitimu Vyuo Vikuu kupata nafasi za kujitolea katika Taasisi, Idara, Mashirika na Mamlaka ya Serikali pamoja na sekta binafsi ili kupata uzoefu. Pamoja na kutazama masharti ya taasisi za kifedha ya upatikanaji wa mikopo ili waweze kujiajiri.
7. Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM limeazimia kwa Kauli moja kumlinda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein dhidi ya uharamia wowote Kutoka ndani au nje ya Tanzania.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Mwl. Raymond S. Mwangwala (MNEC)
KATIBU MKUU
01/09/2018
Post A Comment: