Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2018 Mhandisi Charles Kabeo, ameuagiza uongozi wa wilaya ya Nyamagana chini ya usimamizi wa Dkt Philp Nyimbi kuisimamia halmashauri ya Jiji la Mwanza kujenga vyoo vyenye hadhi na rafiki kwa watu Wote wakiwemo walemavu.
Mhandisi Kabeo ametoa agizo hilo kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Nyamagana katika ukaguzi wa Soko la Kisasa lililojengwa kwa thamani ya shilingi 359,055,679.25 ikiwa mchango wa halmashauri ni shilingi 89,111,179.25 na fedha za wahisani shillingi 269,944,500.00. Mhendisi Kabeo ameelekea ukamilishaji wa miundo mbinu imara na rafiki ya vyoo badala ya kutegemea wawekezaji miundombinu hiyo.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Post A Comment: