Msanii wa muziki Bongo, Dogo Janja amejibu kuhusu taarifa zinazodai kuwa ameachana na mkewe, Irene Uwoya.

Hitmaker huyo wa ngoma kama Kidebe, My Life na nyinginezo amesema kuwa hilo halina ukweli wowote kwa sasa.

"Hatujaachana ni sisi tumeamua kutoweka sana mambo yetu wazi na ndiyo maana unakuta hatuna picha nyingi tulizopiga wote" Dogo Janja ameiambia XXL ya Clouds FM.

Hivi karibuni kumekuwa na minong'ono ya chini kwa chini huwenda wawili hao wameachana mara baada ya Irene Uwoya kuoenekana akila bata pekee yake nchini Dubai.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: