Mapema asubuhi ya leo, Mh Mkuu wa Wilaya ya Pangani - Zainab Abdallah akiambatana na viongozi wa ofisi yake wametembelea shule ambazo zinatarajiwa kufanya mtihani wa darasa la saba leo. Kama inavyo fahamika; kipaumbele cha Kwanza ndani ya Wilaya ya Pangani ni Elimu. Watahiniwa wote walikaa kambi na hivyo ni matarajio ya Wilaya wanafunzi wote watafaulu.

Shule itakayo ongoza kimkoa kutokea Pangani tutaizawadia Photocopy Mashine; na Vijana watakao ingia tatu bora ya Mkoa; tutawazawadia vifaa vyote muhimu vya shule. Na wale watakaofanikiwa kuingia kumi bora kimkoa; uongozi wa Wilaya kupitia Ofisi ya Mbunge itawapeleka Saadani National Park kwa ajili ya kukuza Utalii wa Ndani.

"Tunaamini Elimu ndio urithi pekee wa mtoto wa Mkulima. Kupitia elimu mtoto wa Mama Ntilie anaweza kuwa kiongozi bora na wa mfano katika nchi hii - Mh Jumaa Aweso."

#ElimuKwanza
#PanganiKumenoga
Share To:

msumbanews

Post A Comment: