Septemba 15, 2018 daraja la juu ‘flyover’ lililopo katika makutano ya Tazara lilifunguliwa na magari yakaanza kupita na uzinduzi rasmi unategemea kufanywa na Rais Magufuli mwezi ujao.

Mradi huu ambao ni wa thamani ya Sh bilioni 95 unatekelezwa na kampuni ya Oriental Consultans Global na Eight Japan Engineering Consultants, zote za Japan.

Rais John Magufuli alizindua ujenzi wa ‘flyover’ hii Aprili, 2016 na kueleza kuwa lengo ni kupunguza kero ya foleni jijini Dar es Salaam pindi itakapomalizika na kuanza kutumika.
Picha na Emmanuel Massaka
Share To:

Anonymous

Post A Comment: