Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Craython Revocatus Chipando, maarufu kama Baba Levo aliwasili mapema leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kigoma kusikiliza hukumu ya kesi inayomkabili.

Msanii huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini kwa tiketi ya ACT Wazalendo anatuhumiwa kufanya makosa matatu ikiwemo kutumia lugha ya matusi, kumshambulia na kumfanyia vurugu muuguzi wa zahanati ya Msufini iliyopo kata ya Mwanga Kaskazini.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi terehe 19, Septemba mwaka huu.

Source: Azam TV
Share To:

msumbanews

Post A Comment: