Jopo la majaji wa Tuzo ya Daudi Mwangosi mwaka 2018 limemtangaza Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda kuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2018.
Tuzo hiyo imetangazwa leo Jumanne Septemba 4,2018 wakati wa mkutano mkuu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania UTPC unaofanyika katika ukumbi wa Lush Garden Hotel jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, Ndimara Tegambwage amemtangaza mshindi kisha mgeni rasmi Absalom Kibanda kukabidhi tuzo hiyo kwa mke wa Azory Gwanda ambaye hajulikani alipo tangu Novemba 21,2017.
Mbali na kukabidhiwa tuzo hiyo,pia amekabidhiwa cheti cha utambuzi pamoja na shilingi milioni 10.
Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Kushoto ni Absalom Kibanda akikabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi 2018 kwa mke wa Azory Gwanda
Kushoto ni Absalom Kibanda akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mke wa Azory Gwanda
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, Ndimara Tegambwage akitangaza mshindi wa tuzo ya Mwangosi 2018
Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018
Post A Comment: