Jeshi la polisi Mkoani Pwani, limemkamata Salum Mzee Kondo (38), ambaye ni fundi ujenzi mkazi wa Kidongo Chekundu wilayani Bagamoyo, akituhumiwa kuhusika na tukio la mauaji ya mkewe Mwajuma Omary (27).

Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Septemba 2 mwaka huu, eneo la Yombo Buza jijini Dar es salaam ambako alikimbilia baada ya kufanya kitendo hicho Agosti 31, 2018, saa 9 alasiri huko Kidongo Chekundu.

Kamanda Nyigesa ameweka bayana kuwa mtuhumiwa alipokamatwa alikiri kutenda kosa hilo, na kudai alichukua hatua hiyo kutokana na wivu wa kimapenzi. 

Alisema mkewe alikuwa akichat na simu huku akiwa anacheka mwenyewe ndipo alipoamua kumnyang'anya simu na kukuta akichat na mwanaume mwingine.

Baada ya hapo ulizuka mgogoro mkubwa ambapo walitengena kabla ya Agosti 31 mwaka huu marehemu kumpigia simu mumewe akimdai shilingi elfu 50000 aliyoichukua siku za nyuma bila ridhaa yake, ndipo mme wake akamuita nyumbani akachukue na akatumia mwanya huo kumkaba na kumsababishia kifo.

Kamanda amesema mtuhumiwa huyo aliifunika maiti na kuiacha katika chumba walichokuwa wakiishi kisha kuacha ujumbe ambao ulieleza, amemuua kwasababu ya wivu wa mapenzi na yeye anakwenda kujiua hivyo mali zote walizoacha ni za watoto wawili waliozaa na marehemu.
Share To:

Anonymous

Post A Comment: