TAARIFA KWA UMMA
Kumekuwepo na akaunti feki ya mitandao ya kijamii ya instagram ambayo imesajiliwa kwa jina la ‘‘kangilugola’’ na imekuwa ikitoa taarifa mbalimbali kwa jamii kuhusu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara hii kwa ujumla.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kuujulisha Umma wa Watanzania kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Kangi A. Lugola hana akaunti yoyote kwenye mitandao ya Kijamii hivyo akaunti yoyote iliyosajiliwa kwa jina la kangilugola ni feki.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inatoa onyo kali kwa mtu yeyote anayejihusisha na kutumia jina la Kangi Lugola kusajili akaunti hiyo feki sambamba na kutoa taarifa za Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara kwa ujumla kupitia akaunti hiyo feki, na yeyote atakayebainika kujihusisha na jambo hili hatua za kishera zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha taarifa zote za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zitatolewa kupitia tovuti ya wizara kwa anuani ya www.moha.go.tz na twitter ya Wizara kwa akaunti ya MsemajiMamboyaNdani.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Post A Comment: