Wakazi wa Kisiwa Kodogo Cha Chole Wilaya Ya Mafia Mkoani Pwani Wameiomba Serikali Kufanya Juhudi Za Makusudi Kuiokea Shule Ya Msingi Chole Baada Kuondokewa Na Walimu 4 Na Kubakia Na Walimu Watatu Ambao Hawatoshelezi Mahitaji Halisi Ya Shule Hiyo
Wakingumza Na Global Tv Kijiji Hapo Wamesema Watoto Wao Ambao Wanatarajia Kufanya Mitihani Yao Ya Mwisho , Asa Kwa Wanafunzi Wa Darasa La Saba Wapo Katika Hatari Kubwa Ya Kuferi Mitihani Hiyo Kwa Kuwa Hawapati Vipindi Vya Kutosha Kutokana Na Uhaba huo Wa Walimu.
Shule Hiyo Yenye Mikondo Ya Darasa La Kwanza Mpaka la Saba Imebakiwa Na Waalimu Watatu Kwa Sasa Wanaofundi Baada ya Wangine Wanne Kuomba Uhamisho Kwa Mkupuo Kwa Mujibu Wa Sheria.
Diwani wa Kata Ya Jibondo Bwana Hassani Mohamed Anasema Pamoja Na Mazingira Mazuri Waliyoyaweka Katika Shule Hiyo Yaupatikanaji Wa Maji Na Nyumba Za Walimu Lakini bado Walimu Hao Wameomba Uhamisho Na Kuondoka Zao.
‘’Nilichogundua Tatizo Lipo Kwa Halmashauli Yetu Wamekuwa Wakiwaacha Walimu Wanakaa sehemu Moja Kwa kipindi kirefu uku Visiwani Hali Inayopelekea Waalimu Kuomba Uhamisho Kwa Sababu Wanakosea Mambo Mengi Ya Kujiliwaza Asa Ukizingitia Uku Visiwani Hakuna Vitu Vingi Vya Kujiliwaza’’ Alisema Mhe Diwani Uyo.
Nae Mratibu Elimu Kata Ya Jibondo Khamis Pazi Anasema Shule Hiyo Yenye Mahitaji Ya Walimu 8 Kwa Sasa Inapitia Wakati Mgumu Kwa Kuwa Kitakwimu Shule Hiyo Ina Walimu 4 Kwa Hivi Sasa Lakini Kati Ya Hao Wanne Mmoja Ni Mwalimu Mkuu Ambae Kwa sasa Yupo Likizo Ya Uzazi.
Akielezea Zaidi Mratibu Elimu kata Anasema Waalimu Waliopo Sasa Mmoja Ni Mwalimu Wa Darasa La Awali Na Walimu Wawili Waliobakia Wanafundisha Mikondo Yote Inayobakia Hali Ambayo Inasababisha Kukosa ufanisi Katika Ufanyaji Kazi Wa Kila Siku Hali Inayopelekea Waalimu Waliopo Kubeba Mzigo Mkubwa Wa Vipindi Kila Siku.
Nae Mbunge Wa Jimbo Ilo La Mafia Mbaraka Dau Amesema Kwa Kushirikiana Na Mkurungenzi Wa Hamashauli Hiyo Wanatafuta Ufumbuzi Wa Jambo Ilo Kwa Kujua Idadi Ya Walimu Wanaopatikana Katika Kisiwa Cha Icho Cha Mafia.
Na Kama kuna Shule Ina Waalimu Wengi Wafanye Utaratibu Wa Kuhamishia Shule Ya Msingi Chole Ili Kuziba Nafasi Hizo, Lakini Pia Amewasiliana Na Waziri Seleman Jafo Wa Tamisemi Ambae Ndie Mwenye Dhamana Awapatie Waalimu Ili Kumaliza Tatizo Ilo.
Nae Mkurungenzi Wa Halmashauli Hiyo Mafia Bwana Erick Mapunda Amesema Sababu kubwa Inayosabisha Watumishi Mbalimbali Wanaopangiwa Wilaya Ya Mafia kuomba Kuhama Ni Kutokana Na ukosefu Wa Usafafiri Wa uhakika.
Wilaya Ya Mafia Inakabiliwa Na changamoto Ya Usafiri Kwa Kukosa Meli Inayofanya Kazi kila siku Ambapo Wananchi wa wilaya Hiyo wamekuwa Wakitumia Boti Za Uvuvi ambazo Si Salama Kwa Wasafiri Au Kutumia Ndege Ambazo Gharama Zake Ni Kubwa Ambazo Wananchi Wamekuwa Wakishindwa Kuzimudu
Wilaya Ya Mafia Inakabiliwa Na Kukutwa Na Janga La Ukosefu Wa Watumishi Kwa Kuwa Kwa Mujibu Wa Mgurungenzi wa Halmashauli Erick Mapunda Anasema Maombi Ya Watumishi Wanaomba Kuhama Ni Mengi Kuliko Wanaingia Wilayani Mafia, Ambapo Wilaya Hiyo Mpaka Sasa Ina Mapungufu Ya Ya Watumishi Katika Idala Ya Elimu Ya Waalimu 119, Na waliopo Ni 257, Na Mahitaji Wilaya hiyo Hinahitaji Jumala Ya Waalimu 373 Kutosheleza Shule 6 Za Sekondali Moja Ya Kidato Cha Tano Na Shule Za Msingi 15
Post A Comment: