Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa amembeba mtoto aliyeletwa Kliniki katika kituo cha afya Mto wa mbu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akisalimiana na wananchi wa mto wa mbu wilayani Monduli.
Wananchi wa mto wa mbu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo.
Viongozi wakiwa eneo la Makuyuni wakikagua ujenzi wa miundombinu ya kituo cha Afya Makuyuni.
Wananchi wa Mto wa mbu na Makuyuni wilayani Monduli Mkoani Arusha wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kwa uboreshaji wa huduma za afya wilayani humo. Wananchi hao wametoa pongezi hizo katika ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri Jafo anakagua miradi ya maendeleo na kufanya ufuatiliaji wa maagizo yake aliyo yatoa miezi ya nyuma katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo kwasasa ametokea mikoa ya Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera, na kigoma. Hatua ya ziara hiyo ilitokana hivi karibuni serikali imepeleka fedha katika kituo cha afya Mtowambu kiasi cha shilingi milioni 400 na baadae imepeleka fedha zingine shilingi milioni 400 katika kituo cha afya Makuyuni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.
Katika ziara ya Waziri hiyo wilayani Monduli, Wananchi hao wameishukuru serikali na kwamba hatua hiyo itaboresha na kuwezesha huduma bora kutolewa kwenye vituo hivyo. Wamesema ukosefu wa vituo hivyo uliwafanya kukosa huduma za upasuaji. Kwa upande wake, Waziri Jafo amemshukuru aliyekuwa mbunge wa Monduli Julius Kalanga kwa kufikisha kero za wananchi wa Monduli katika Ofisi yake na serikali ikapeleka fedha hizo ili kuwasaidia wananchi hao ambao walikuwa wakitaabika miaka yote bila ya kuwa na vituo vya afya vinavyoweza kufanya huduma ya upasuaji. Jafo amewapongeza sana wananchi hao kwa kuungana na serikali na kufanikisha uboreshaji wa kituo cha afya mtowambu pamoja na juhudi za ujenzi zinazo endelea katika kituo cha afya Makuyuni.
Aidha Waziri Jafo amewajulisha wananchi hao kwamba serikali itapeleka vifaa tiba vyote katika kituo cha afya Mtowambu ambacho tayari kimekamilika ili wananchi hao wapate kuonja matunda mazuri ya utekelezaji wa Ilani ya CCM. Katika ziara hiyo Jafo amewataka viongozi walio chini ya Ofisi yake kuanzia mikoani hadi wilayani wahakikishe wanajituma muda wote katika maeneo yao kwa lengo la kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Post A Comment: