Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amewataka watumishi wa Kituo cha Afya cha Usa-River, kuwahudumia wagonjwa wanaofika kituoni hapo kwa kuzingatia maadili ya utabibu yanayo sisitiza kutoa huduma Kwa viwango bora na Kwa wakati.  
Akiongea na watumishi wa kituo hicho amefafanua kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi hivyo hawanabudi kuwahudumia wananchi hao Kwa huduma stahiki na Kwa wakati kama miongozo ya kitabibu inavyotaka.  "Serikali ilitoa milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo  mapya kituoni hapo ambayo ni jengo la maabara,nyumba ya mtumishi, jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto, chumba cha kuhifadhia maiti, kichomea taka pamoja na kufanya ukarabati wa majengo yaliyokuwepo kwa lengo la kuwapa wananchi huduma bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

Mkurugenzi Kazeri amewaonya watumishi wa kituo hicho  ambao hutumia lugha isiyo ya staha Kwa wagonjwa pamoja  na wanaopokea  rushwa kwa wagonjwa kuacha mara moja, kwani Serikali haitawavumilia mtumishi wa namna hiyo ambaye anakwenda na kinyume cha maadili ya utabibu pamoja na azma ya serikali ya kutoa huduma bora ya Afya Kwa wananchi ,""amesema Kazeri.     

Kazeri ameongeza kuna umuhimu kwa wasimamizi wa kituo hicho kupanga utaratibu utakaowezesha vikao vya asubuhi  kutokuwa sababu ya wagonjwa kukosa huduma. 

Naye Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dkt. Aggrey Kibutu amemthibitishia Mkurugenzi huyo kutekeleza maagizo yake kwa  kutoa huduma bora Kwa wananchi Kwa kuwa wanatambua dhamira ya serikali katika kuboresha huduma ya Afya nchini.  "Kituo Chetu kina watumishi wengi wapya ambao wamehamishiwa hapa lakini tunaendelea kujipanga kwani idadi ya wagonjwa tayari imeongezeka  mara tatu katika  kituo cha Afya Usa –River , na hii ni baada ya   uboreshaji  wa miundombinu , ambapo idadi ya wagonjwa wa nje (out patient) imeongezeka kutoka wagonjwa   600  kwa mwezi hadi  wagonjwa 2000 na zaidi kwa mwezi,  hivyo tunakuahidi kuboresha utendaji kazi wetu Kwa watakao fika kupata huduma" Amesema Kibutu
Mkugenzi wa Halmashauri hiyo ametembelea kituo hicho  ikiwa  Ni Sehemu ya kuhakikisha watendaji wa Halmashauri hiyo  wanatekeleza majukumu yao na wananchi wanapata huduma bora.
PICHA ZA TUKIO.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri  ya Wilaya ya Meru Christopher Kazer akizungumza na watumishi wa  wa kituo cha Afya Usa- River.
Watumishi wa  wa kituo cha Afya Usa- River wakifuatilia kwa makini mazungumzo wakati wa kikao baina yao na Mkurugenzi Kazeri.
Mganga mfawidhi wa kituo  kituo cha Afya Usa- River ,Dkt. Aggrey Kibutu akizungumza katika kikao cha Mkurugezi wa Halmashauri ya Meru na watumishi wa kituo hicho.
Watumishi wa  wa kituo cha Afya Usa- River wakifuatilia kwa makini mazungumzo wakati wa kikao baina yao na Mkurugenzi Kazeri.
Kushoyo kwa Mkurugenzi Kazeri niMkuu wa idara yautawala Grace Mbilinyi na kulia kwa Mkurugenzi ni Afisa utumishi Edward Chitete.
Watumishi wa  wa kituo cha Afya Usa- River wakifuatilia kwa makini mazungumzo wakati wa kikao baina yao na Mkurugenzi Kazeri.
Watumishi wa  wa kituo cha Afya Usa- River wakifuatilia kwa makini mazungumzo wakati wa kikao baina yao na Mkurugenzi Kazeri.
Watumishi wa  wa kituo cha Afya Usa- River wakifuatilia kwa makini mazungumzo wakati wa kikao baina yao na Mkurugenzi Kazeri.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: