Mgeni rasmi Afisa Ushirika Jiji la Arusha Huruma Kibendwa akimkabidhi cheti mmoja wa kundi la Kanono, aliyepo kushotonkwake ni Mwenyekiti wa Kundi la Kanono Wilbald Ngambeki, na wakwanza kulia ni Davis Kalegea mtendaji wa kundi hilo. IMG_20180826_123620
Wakina mama pamoja na wanaume kutoka kabila la Wanyambo waishio mkoani Arusha wakifanya maandalizi ya kutengeneza vyakula vya asili katika tamasha hilo. Picha na Vero IgnatusIMG_20180826_123754
Maandalizi ya chakula cha asili yakiendelea kama inavyoonekana pichani.IMG_20180826_123755
IMG_20180826_123907
Tayari unga wa muhogo umeshapatikana kwaajili ya kupika maandazi ya asili ya watuIMG_20180826_123429
Maandalizi ya juice ya asili ikiendelea.IMG_20180826_124151
Juice ya asil iliyoandaliwa na wakina mama wa kabila la Kinyambo katika tamasha hiloIMG_20180826_130810
Ngoma ya asili ya Kabila la Wanyambo wakitumbuiza katika tamasha hilo. Picha na Vero Ignatus.


Na. Vero Ignatus. ARUSHA


Watanzania wameshauriwa kuenzi mila na desturi nzuri ili kuzirithisha kwa vizazi vijavyo na kuwa na Taifa lenye utamaduni madhubuti. 

Rai hiyo imetolewa katika tamasha linalokutanisha familia 172 zenye jumla ya watu 323 kutoka katika kabila la wanyambo kutoka wilaya za Karagwe na Kerwa waishiao mkoani Arusha. Akizungumzia lengo la tamasha hilo mwenyekiti kikundi cha Kanono Wilbard Ngambeki amesema lengo kubwa ni kuimarisha umoja na kuzifanya familia zilizozaliwa kufahamu tamaduni zile nzuri za wazazi wao. 

'' Katika tamasha hili michezo imekuwa ni kivutio kikubwa, wazazi wanawaleta watoto wao ila sisi tunapitisha mila zetu na desturi zetu njema kwao ili wakue wakitambua wazazi wao ndipo tulipotoka hata watakapokuwa kwenye miji mingine ya watu mbali na wazazi wao.''

Ngambeki amesema umoja huo wa Kundi la Kanono tayari walishaanzisha Saccos ambayo inawanachama 105 waliojiunga na tayari wameshakopeshana zaidi ya milioni 800 kwa riba nafuu. Afisa Ushirika Jiji la Arusha Huruma Kibendwa aliyekuwa mgeni rasmi katika tamashaa hilo amepongeza umoja kwa kuwa na saccos ambayo inawasaidia kukopeshana wao kwawao na kujikwamua kiuchumi na kimaendeleo

'' Kwani mara nyingi tunawashauri wanamchi wajiunge kwenye vikundi ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kukopeshana wao kwa wao mkopo wenye riba nafuu uzuri kikundi hiki kimesajiliwa na mna saccos inayofanya vizuri '' Alisema Kibendwa. 

David Igola ni mmoja wa wa wanakanono amesema kuwa zipo faida kubwa ambazo amezipata katika kundi hilo ikiwemo kuenzi mila na desturi nzuri za kabila hilo, ikiwemo kusaidiana katika nyanja mbalimbali kama vile elimu, matibabu, shughuli za kijamii na nyinginezo nyingi. 

'' Sanasana ukiangalia vile vitu vya asili tunavyokuanavyo, watoto wetu ambao wengi wamezaliwa mjini wengi hawavuelewi unakuta tunapokwenda nao vijijini wengi wanavushangaa, ila kwenye tamasha kama hili vinatengenezwa wazi na wanajifunza''Alisema Igola. Tamasha hilo limeambatana na michezo mbalimbali iliwemo ya ngoma za asili, mapishi ya asili, kuvuta kamba kukimbiza kuku, ngonjera pamoja na ushairi. 




Kundi hilo la Kanono lilianzishwa rasmi 1996 na kupata usajili 27August 2012 ambapo Jina Kanono ni heshima kutoka kwa kiongozi wao Omkama.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: