Na James Timber, Mwanza
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa Mwanza wameshangilia ujio wa Mwenge wa Uhuru wakati wa makabidhiano na Mkoa wa Shinyanga mapema hii leo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Izizimba A wilayani Kwimba.
Mwenge huo unatarajia kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 13.
Kiiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Charles Kabeho amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kwa mapokezi makubwa na kuahidi kukagua miradi yote iliyokusudiwa hatua kwa hatua ili kujiridhisha ubora wa utekelezaji wake.
Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Mwanza zinatarajiwa kufikia tamati Siku ya Jumapili Tarehe 2 Septemba, Mwaka huu ambapo utakabidhiwa katika Mkoa wa Mara.
Post A Comment: