Na Frankius
Cleophace Tarime.
Viongozi wa
CHADEMA Wilaya ya Tarime pamoja na Wabunge akiwemo Mbunge wa Jimbo la Tarime
Mjini Esther Matiko, Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA Mkoa wa Mara Joyce Sokombi na Makamu Mwenyekiti kanda ya Serengeti CHADEMA ambaye ni Mbunge Viti
Maalum Mkoa wa Simiyu Gimbi Masaba pamoja na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mara Mwl
Chacha Heche na Viongozi Wa chmaa hicho
na Mawakala wameweka kambi takribani masaa manne katika ofisi ya kata ya Turwa kwa
ajili ya kushinikinikiza mawakala wao waweze kuapishwa kwa mujibu wa kanuni ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.
Akiongea na
Waandishi wa habari katibu wa CHDEMA Mkoa wa Mara Mwl: Chacha Heche amesema
kuwa Viongozi ambao ni wasimamizi wa uchaguzi mdogo kata ya Turwa tangu asbuhi
wamekuwa wakiwazungusha huku na kule ili
kupoteza muda wao na ili mawakala wao wasiapishwe kwa Mujibu wa Sheria jambo
ambalo wamedai hawatakubaliana nalo.
“Kanuni za
Uchaguzi zinataka Vyama vya Siasa kupeleka Mawakala kwa Msimamizi Mkuu wa
Uchaguzi au msaidizi ili kuwaapisha kabla ya siku saba za uchaguzi lakini sisi tumefanya hivyo tangu asbuhi
mpaka sasa hakuna chochote Mkurugenzi wa mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa
tumeenda Ofisini kwake hajafanya chochote mpaka sasa lakini kama chama
tumeamwandikia barua ili atupe sababu kwa maandishi kwanini hataki kuapisha
Mawakala hawa” alisema Chacha.
Kwa upande
wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini CHADEMA Esther Matiko amesema kuwa
viongozi wote wameshinda katani hapo badala ya kwenda kufanya shughuli za
Maendeleo kwa sababu ya Kiongozi wa Serikali kushindwa kutimiza wajibu wake hivyo amesema
kuwa wataendelea kiukaa maeneo hayo mpaka Majira ya saa Kumi Jioni kama
hawajajibiwa kwa Maandhi kwanini Mawakala hawajaapishwa wataripoti Maeneo
huska.
“Viongozi
Wachache wanaotaka kupindisha Mambo ndo wanaweza kusababisha Vurugu Tarime na
sisi kama Viongozi wa Wananchi hatutaki wananchi kuumia sasa waachea waananchi
wakachague Viongozi wao” alisema Matiko .
Mpaka habari
hii inaenda hewani bado viongozi wa CHADEMA walikuwa bado wameweka kambi katika
Ofisi za CHADEMA ili kupatiwa ufumbuzi wa jambo hilo.
Post A Comment: