Timu ya riadha Arusha ikiwa na Uongozi wa riadha wa mkoa pamoja pia na kaimu kamnda wa Jeshi la polisi Yusuph Ilembo.
Wafukuza
upepo wa jeshi la polisi mkoani Arusha wameagwa rasmi hii leo kwa ajili ya
kuanza safari ya kuelekea Jijini Dar es salaam katika mashindano ya majeshi ambayo yanataraji kushirikisha mataifa
mbalimbali ya nchi za ukanda wa maziwa makuu.
Akizungumza
na wanariadha hao kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha yusuph ilembo
amewataka wafukuza upepo hao kwenda kufanya vyema na kuhakikisha kuwa medali
hizo zinasalia hapa nchini.
Katibu mkuu
wa chama cha riadha mkoani Arusha Alfredo Shehanga pamoja na afsa michezo chuo
cha polisi moshi Emanuel mtatifikolo wanasema maandalizi ya wanariadha hao
yamekamilika na kuahidi kuwa baada ya wanariadha hao kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya mwaka jana sasa ni nafasi ya wanariadha hao kufanya vyema katika mashindano hayo.
Nchi za Maziwa Makuu ni nchi zinazopakana na maziwa makubwa ya Afrika ya mashariki pamoja pia na nchi jirani na mataifa hayo ya Afrika
mashariki zikiwa zimezungukwa na maziwa makubwa ya ziwa Tanganyika,ziwa Victoria,ziwa
albert,ziwa Edward ziwa kivu pamoja na ziwa Nyasa.
Timu hiyo ya jeshi la polisi Arusha ipo chini ya mwalimu Rogath John
Post A Comment: