TUME YA NGUVU ZA ATOMU TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
Teknolojia ya Nyuklia inavyoweza Kutumika Katika Sekta ya
Kilimo na Mifugo ili kukuza uchumi wa Biashara Na Viwanda
Arusha,
Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania inashiriki maonesho kilimo katika viwanja vya TASO
nanenane jijini Arusha, Maonesho haya yaliyoanza rasmi tarehe 01 Agosti, 2018 yanatoa
fursa kwa Tume kutoa elimu juu ya udhibiti wa viasilia vya mionzi vinavyoweza kupatikana
kwenye mazao ya chakula na mifugo ili kuongeza usalama wa mtumiaji dhidi ya madhara hatari
yanayoweza kusababishwa na mionzi.
Katika maonesho haya Tume inatoa elimu juu ya teknolojia ya nyuklia inavyoweza kuwa
mkombozi kwenye ukuaji wa uchumi wa biashara na viwanda ikilengea matumizi salama ya
teknolojia hii hapa nchini ili kuboresha na kuongeza ustawi kwenye sekta za Afya, Maji, Kilimo,
Nishati na Mifugo .
Katika hatua za awali Tume imeshafanya upembuzi yakinifu wa kutumia teknolojia ya
nyuklia/mionzi katika kuhifadhi vyakula, mazao na kuboresha bidhaa za viwandani ili kuzipa
muda mkubwa wa matumizi na kuzikinga dhidi ya uharibifu unaoweza kusababishwa na
bacteria
Teknolojia ya nyuklia ina mchango mkubwa sana katika sekta ya kilimo na mazao ya mifugo
kwani uhakikisha bidhaa zitokanazo na mazao haya zinakuwa bora na za uhakika ili kuboresha
afya ya mlaji
Teknolojia ya nyuklia imeridhiwa kimataifa na inatumika katika nchi zaidi ya 60 duniani kote
katika kuua bacteria na vijidudu katika vyakula, matunda na mazao, kuifadhi kwa muda mazao
yasiharibike, kuua vijidudu katika bidhaa za viungo (Spices),teknolojia hii pia hutumika katika
kuzuia vijidudu kwenye nyama na samaki mfano (Salmonera, Ecoli, Trichinosi), kuongeza ubora
wa bidhaa za vyakula kwa kuvifanya visiharibike mapema, kuzuia viazi vitunguu na bidhaa
zingine zisiote wakati zikiwa zimehifadhiwa.
Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 30% ya vyakula duniani vinaharibika kila mwaka
kwa sababu ya kuaribiwa na vijidudu au kuoza, upotevu au kuharibika kwa chakula kuna athari
kubwa katika kipato na maisha ya wakulima kwa mfano inakadiriwa kwamba kila mwaka
hasara inayotokana na kuharibika kwa mazao ya nafaka barani Afrika hasa kusini mwa jangwa la
Sahara inafikia dola za kimarekani bilioni 4 na hii ni sawa na asilimia 15 ya thamani ya mavuno
hayo, sambamba na matukio ya binadamu kuambukizwa vijidudu vya salmonella yanafikia hadi
idadi ya watu wapatao 120,000 kila mwaka ambapo maambuki haya ya bacteria yamekuwa
yakisababisha vifo vingi.
Gharama za matibabu yanayosababishwa na madhara ya maambukizi haya ya vijidudu vya
salmonella na Ecoli yamekuwa yakisababisha hasara ya Dola za kimarekani bilioni 6 kila mwaka.
Teknolojia ya nyuklia endapo itatumika kwa usalama kwa kuzingatia matakwa yote ya kanuni za
usalama na ubora wa bidhaa na vyakula itakuwa suluhisho la kudumu kwenye sekta ya kilimo
na mifugo, kwani teknolojia hii ni salama na ya uhakika, hakuna athari zozote zitokanazo na
teknolojia hii wala chembe chembe za mionzi zinazoweza kubakia kwenye vyakula wakati wa
zoezi la mnyunyulisho (Food Iradiation).
Wananchi wote hususani wakazi wa Jiji la Arusha mnaombwa kufika kwenye banda la Tume
lililopo karibu na jukwaa kuu ili mjipatie elimu juu ya huduma zinazotolea na Tume ya Nguvu
za Atomu Tanzania pia kujionea majukumu yanayotekelezwa Kisheria kwenye usimamizi na
udhibiti wa mionzi hapa nchini ili kulinda mazingira, wananchi na wafanyakazi wanaotumia
vyanzo vya miozni katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Teknolojia ya Nyuklia kwa Maendeleo ya Taifa”
Imetolewa na
Peter G. Ngamilo
Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania
Post A Comment: