Na Ferdinand Shayo, Arusha.
Shirika la umeme mkoani Arusha Tanesco limetaadharisha wanaohujumu miundombinu ya umeme na kulisababishia Shirika ilo hasara ikiwemo kuchakachua mita ili kukwepa kulipa gharama za huduma hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Tanesco Mkoa wa Arusha Saidi Mremi amesema kuwa kwa sasa wanateknolojia za kuweza kubaini iwapo mita imechezewa na wamekua wakiwachukulia hatua wale wote waliobainika kuhujumu miundombinu ya Tanesco.
Aidha amesema kuwa wameendelea kufanya ukaguzi na operesheni mbalimbali ambazo zimekua zikifanyika Mara kwa Mara ili kuwabaini wanaohujumu juhudi za tanesco kuwafikishia wananchi umeme.
Msimamizi wa kitengo Charles John amesema kuwa wamekua na mfumo mzuri wa ufuatiliaji wa mita Za umeme ambao umekua Ukisaidia katika kuhakikisha kuwa wananchi wanalipia huduma Huyo..
Kwa upande wao wananchi wa jiji la Arusha Khalfani Saidi ,Richard Msechu.wameiomba Tanesco kusambaza umeme katika maeneo ambayo bado na pia wamesema kuwa wako tayari kushirikiana na Tanesco Katika kuwabaini wanaohujumu Shirika hilo na kusababishia serikali hasara.
Post A Comment: