Ni shirika la New Dawn Communities linalofanya kazi kata ya Njoro iliyoko Wilayani Same kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo toka Califonia nchini Marekani.
Shule inategemea kupokea watoto yatima na walemavu kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita.
Jiwe la msingi upande wa mabweni lawekwa na DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule na Mch. Ron kutoka Marekani ambapo linategemea kupokea wanafunzi kuanzia Januari, 2019.
Wadau wapania kujenga pia tawi la Chuo kikuu cha Pippeliner (kilichopo Marekani) katika eneo hilo. Waanza kushirikisha waliosoma chuo hicho kuchangia.
DC Same awakumbusha kufuata sheria na taratibu za nchi zinazohusiana na mradi huo. Awaasa kuweka utaratibu mzuri wa kuwapata watoto hao; Atoa wito kwa wazazi na wananchi kutumia fursa hiyo badala ya kuwafungia watoto walemavu nyumbani.
Mch. Mshomi ambaye ndiye mkurugenzi wa taasisi hiyo, amesema wanategemea kupokea wanafunzi zaidi ya 600 wenye uhitaji na kuwasomesha. Pia wanaendelea kushirikiana na jamii kwa huduma nyingine kama kilimo cha bustani, huduma ya maji bure, ujenzi wa barabara na wamekusudia kujenga uwanja wa kisasa wa mpira. Aiomba jamii kuwapa ushirikiano.
" Nawashukuru kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bure na sera ya nchi inayotoa haki sawa ya elimu kwa watoto wakiwemo yatima na walemavu, asanteni sana". Alisema DC Same.
Post A Comment: