Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako amesema
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuimarisha ubora wa
elimu katika ngazi zote .
Waziri
Ndalichako amesema hayo alipokuwa akizindua Jengo Jipya la Hosteli ya
Wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya
Kigamboni.
Profesa
Ndalichako amesema kuwa pamoja na kujikita kwenye kujenga maadili na
uzalendo katika chuo hicho pia amewaagiza kuwa wanahakikisha wanaandaa
wanafunzi mahiri na wenye ujuzi utakaowawezesha kuchangia katika uchumi
wetu.
“
Ubora wa elimu inayotolewa na Chuo chenu uwe ni wa kiwango cha juu
kinachokubalika kitaifa na kimataifa. Na kwa kufanya hivyo mtakuwa pia
mmetekeleza Dira yenu ya Elimu ambayo kama Taifa tunataka kuwa na
Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na
mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika maendeleo ya Taifa”Amesema
Ndalichako.
Waziri
Ndalichako amesema Mafanikio ya chuo pamoja na ujenzi wa hostel hiyo ya
wanafunzi kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Chuo ni sehemu ya
utekelezaji wa Dira ya chuo na pia ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi na
Ilani ya uchaguzi ya chama Tawala cha Mapinduzi.
Aidha
alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk .John Pombe Magufuli kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa
Ilani ya CCM, hivyo kuendelea kujenga imani kwa Watanzania ambao ndiyo
waliyompa ridhaa kuongoza nchi yetu.
“Leo
hii tunashuhudia uzinduzi wa Hostel hii ambayo ilianza kujengwa Aprili
2012 na ilipaswa kukamilika Januari 2014. Hata hivyo, ujenzi huo ulikuwa
umesimama kutokana na ukosefu wa fedha.
Tunamshukuru
sana Rais ambaye alitembelea Chuo hiki mwezi Agosti 2017 na kuahidi
kuwa atahakikisha Shilingi 1,189,000,000 zilizokuwa zinahitajika kwa
ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hili zinapatikana. Kama ilivyo
kawaida yake, Mheshimiwa Rais akiahidi anatekeleza, fedha zilipatikana
na ujenzi uliokuwa umesimama tangu mwaka 2014 sasa umekamilika na tuko
hapa kwa kuzinduzi rasmi wa jengo hilo.
Mheshimiwa
Rais alipenda sana aje mwenyewe kuzindua, lakini kutokana na majukumu
mengi aliyonayo amenituma nifanye kazi hii. Anawapongeza sana kwa
kusimamia vizuri kazi hii” Amesema Waziri Ndalichako.
Kwa
Upande wake Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa
Shadrack Mwakalila amesema Hostel hiyo mpya itasaidia kupunguza tatizo
la malazi, hivyo kuwapa wanachuo mahali pazuri na salama pa kuishi na
kuwaongezea muda wa kujisomea.
Amesema
kuwa Hoteli hiyo ambayo inachukua wanafunzi Zaidi ya 700 itaweza
kukamilisha idadi ya wanafunzi watakaokuwa wanalala shuleni hapo kuwa
Zaidi ya 1000 Hivyo, ni muhimu itunzwe vizuri ili iendelee kuwanufaisha
wanafunzi wengi zaidi kwa miaka ijayo.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akizungumza
na Wanafunzi na wagaeni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa jengo
jipya la chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kigamboni
Jijini Dar es Salaam
MKuu
wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ,Profesa Shadrack Mwakalila
akizungumza juu ya historia ya ujezni wa Hosteli hizo.
Kaimu
Mwenyekiti wa bodi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Mashavu
Ahmad Fakhi akizungumza kwa Niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Hicho
,Profesa Mark Mwandosya.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako kushoto ni
Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Profesa Shadrack
Mwakalila na Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa bodi wa Chuo Cha Kumbukumbu
ya Mwalimu Nyerere , Mashavu Ahmad Fakhi wakikata utepe kuashiria
uzinduzi wa jengo jipya la hosteli ya Wanafunzi
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akipeana
mkono wa pongezi na Kaimu Mwenyekiti wa bodi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere , Mashavu Ahmad Fakhi mara baada ya kuzindua jiwe la
Msingi
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akikata utepe
kabla ya kuingia kukagua jengo jipya la Hosteli ya Wanafunzi.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akiwa ndani
akikagua kwa makini Vitanda na thamani zilizopo ndani ya Hosteli hizo.
Sehemu
ya Jengo Jipya la Hosteli ya Wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere Likionekana kwa nje mara baada ya kuzinduliwa na Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa bodi wa chuo hicho
Post A Comment: