Kifo cha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), Mtawa Suzan Bartholomew (48), aliyefariki dunia baada kujirusha kutoka ghorofa ya tano kinadaiwa kutokea baada ya kubainika kwa hasara ya zaidi ya Sh milioni 380 mali ya hospitali hiyo.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya hospitali hiyo ya Bugando na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna zimeeleza kuwa mtawa huyo aliamua kujirusha ili kujiua kutokana na kukabiliwa na kesi ya upotevu wa fedha kiasi cha Sh milioni 380.

Kamanda Shana amesema siku chache kabla ya kifo chake mtawa huyo alikamatwa na kuhojiwa pamoja na watumishi wengine nane ambao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha zaidi ya Sh milioni 380 za hospitali hiyo.

“Hadi sasa tunaweza kusema kifo chake kimetokana na tukio la upotevu wa fedha katika ofisi yake, akiwa kama mkuu wa kitengo cha fedha tulimkamata na kumhoji kwa siku kadhaa kuhusiana na upotevu huo wa fedha na kumuachia kwa dhamana, hivyo wakati akijirusha kujiua alikuwa nje kwa dhamana,” amefafanua.
Share To:

Anonymous

Post A Comment: