Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti amewahatadharisha wafuasi wa chadema waliopanga kufanya fujo kuwa jeshi la polisi limejipanga kukabiliana na yeyote atakaejaribu kuvuruga amani katika siku ya uchaguzi mdogo wa marudio kesho Agosti 12.2018.

Amesema kuwa serikali pamoja na jeshi la polisi vipo imara hivyo watu waende kupiga kura bila wasi wasi kwani ulinzi ni asilimia mia moja 100%.

Akizungumza wakati wa kampeni za mwisho za kumnadi mgombea wa Ccm kata ya Bagara Nikodemus Bonifasi  [Nyeusi] alieleza kuwa ilani inayotekelezwa ni ya Chama cha Mapinduzi pekee hivyo vyama pinzani ni wasindizaji.

Mnyeti amesema baada ya uchaguzi kesho ataambatana na diwani wa kata ya Bagara na kutatua changamoto za ardhi zilizopo katika kata ya Bagara.

Ikumbukwe kwamba uchaguzi mdogo wa marudio kwa madiwani unafanyika jumapili kesho baada ya madiwani wengi wao wakiwa ni wa Chadema kukihama chama hicho na kuhamia Ccm.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: