Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akikata utepe kwaajili ya ufunguzi wa ujenzi wa barabara za Manispaa ya Bukoba kwa Kiwango cha lami Nzito
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akikagua barabara inayotarajiwa kuanza ujenzi wake kwa kiwango cha lami hivi karibuni kabla ya kuweka jiwe la ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiongea na wananchi(hawapo pichani) mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za manispaa ya Bukoba kwa kiwango cha lami nzito.
MKUU wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami nzito zenye urefu wa kilometa tano katika Manispaa ya Bukoba.
Mradi huo utagharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3 hadi utakapokamilika Mwezi April 2019.
Gaguti alimtaka Mkandarasi NCL INTERNATIONAL LIMITED kutekeleza mradi huo kwa kiwango kinachotakiwa na kuukamilisha kwa muda uliopangwa au ikiwezekana aukamilishe kabla ya muda ili wananchi wawanufaike na mradi huo mapema zaidi.
Alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanausimamia mradi huo pamoja na kuwa mradi huo una wasimamizi na wataalamu lakini pia wananchi wana wajibu wa kutoa taarifa watakapoona hawaridhishwi na kazi zinazotekelezwa na Mkandarasi watoe taarifa mara moja kwani mwisho wa siku mradi huo utabaki kuwa wa kwao na ndio wanufaika.
"Ndugu zangu wananchi mkiona mambo yanaenda sivyo toeni taarifa mara moja ili hatua sitahiki ziweze kuchukuliwa,mradi huu ni wenu na nyinyi ndo wanufaika"alisema Gaguti
Mradi wa ujenzi wa barabara katika Manispaa ya Bukoba umegawanyika katika sehemu kuu nne ili kukamilisha kilometa tano ambapo kilometa 1.7 ni barabara ya Nshambya KCDP itakayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.1 pia kuna kipande cha Show kilometa 1.05, Nyangoye kupita Halmashauri ya Bukoba (Chemba) kilometa 1.3 na kipande cha kilometa 1.95 cha Bin Said hadi Kilimahewa. Barabara zote zenye urefu wa jumla ya kilometa 5 zitagharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3
Fedha za kutekeleza mradi huo wa kuimarisha miundombinu ya barabara mijini ilitolewa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo muda wa utekelezaji wa mradi ni kuanzia Juni 18, 2018 hadi Aprili 17, 2019 ambapo kazi ziatakazofanyika ni kujenga makaravati 17, mifereji ya maji, kuweka rami nzito na kujenga daraja moja eneo la barabara ya kuelekea ziwani.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkao Gaguti alitembelea kiwanda cha BUKOP cha kukoboa kahawa kujionea ukoboaji wa kahawa unavyoendelea, Pia litembelea mradi wa BUWASA wa upanuzi wa huduma za maji Ihungo na kukagua Ujenzi wa madarasa yaliyofadhiliwa na Serikali ya Watu wa Japani katika Shule za Msingi Kashozi na Nyakato Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, mwisho aliongea na kujitambulisha kwa. watumisha wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Manispaa ya Bukoba na wadau. mbalimbali wa maendeleo katika ukumbi wa chemba Bukoba Vijijini
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za lami nzito zenye urefu wa kilometa tano katika Manispaa ya Bukoba
Post A Comment: