Rais John Magufuli, amewaambia Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Makatibu Wakuu alikaa na majina yao kwa muda wa miezi mine kabla ya kuwateua kushika nafasi hizo.
Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi hao leo Jumatano Agosti Mosi, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewataka viongozi hao kutambua ni Mungu ndiye amewachagua.
“Nimekaa na majina yenu zaidi ya miezi minne, wengine wamepungua wengine wameongezeka.
“Tanzania ni kubwa mno, mimi sikufaa kuwa rais, ni Mungu alitaka na ndiyo sababu siwezi nikasimamam nikajisifu, ni Mungu alitaka vile vile Makamu wa Rais.
“Hata Waziri Mkuu… kwanza hata sijui nilimchaguaje, kwa sababu kuna watu walikwenda Dodoma na suti wameshona ili wawe Waziri Mkuu, lakini Majaliwa (Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa) ni Mungu aliamua awe Waziri Mkuu, vivyo hivyo katika nafasi zenu,” amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli pia amesema nafasi hizo kwa viongozi hao, zimepangwa na Mungu ambaye alitaka wazipate ambapo wakiamini hivyo kila mmoja katika nafasi yake atatenda haki kwa wakati wake.
“Wengine wanasema nimechagua wapinzani, nani mpinzani Tanzania hii, Kafulila (David Kafulila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe) mtasema ni mpinzani.
“Alipokuwa huko alipigania suala la IPTL, akaitwa tumbili leo umteue useme umeteua mpinzani, huyu si mpinzani ni mpiganaji wa serikali yake,” amesema
Post A Comment: