Watu wawili, Benedicto Kalimila (65), mkazi wa kijiji cha Bwanga wilayani Chato na Theodora Charles (62), mkazi wa Kijiji cha Lwamgasa, Geita, wamefariki dunia papo hapo baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua.


Kalimila na Charles walikumbwa na mkasa huo katika kijiji cha Lwamgasa wakati wakichenjua mchanga wa dhahabu kwa kutumia karai.

Diwani wa Lwamgasa, Dotto Kaparatus, alisema juzi kuwa, tukio hilo lilitokea Agosti 22, mwaka huu saa nane mchana.

Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilisababisha hisia tofauti kiasi cha ndugu Benedicto kuzuia mwili wa ndugu yao kuondolewa eneo la tukio mpaka kwanza aletwe mganga wa kienyeji ili kuuondolea mkosi pamoja na waliougusa.

Mashuhuda hao, akiwamo Fitina Seleman, ambaye ni mtoto wa marehemu Charles, aliyekuwapo wakati tukio hilo likitokea,walisema radi ilipiga nyumbani kwa Benedicto mara ya kwanza na kuvuunja mti na kupasua ndoo ya plastiki iliyokuwa na maji.

Fitina aliongeza kuwa kwa mara pili radi hiyo ndiyo ilipiga eneo walilokuwapo wote yeye akiwa pembeni na ndipo ilipowapiga wote na Kilamila na Charles walipoteza maisha papo hapo.
Chanzo - Nipashe
Share To:

Anonymous

Post A Comment: