JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kukamata gari aina ya V8 Nissan Patrol linalodaiwa kuwa la wizi na kuwekwa namba bandia za usajili T 194 DEO .
Kamanda Issah alisema Gari hilo linadaiwa kupotea Nairobi nchini Kenya huku likitajwa kuwa ni mali ya mfanyabiashara mkubwa wa nchini humo kabla ya kukamatwa katika kizuizi cha asakri kilichopo jirani na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA ) eneo la kwa Wasomali.
"Tumekamata gari ambalo limeibiwa huko Kenya na tunawashikiliwa watu wawili ambao wanadaiwa kuhusika na wizi wa gari hilo. Tunategemea kulikabidhi kwa wahusika na hao watuhumiwa watapelekw Kenya kujibu mashtaka yao"alisema Kamanda Issah.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Hamis Issa aikionesha kwa waandishi wa Habari Gari aina ya Nissan Patrol v8 linalodaiwa kuibiwa Nairobi nchini Kenya kabla ya kukamatwa likiwa njiani kuelekea jijini Arusha.
Muonekano wa Ndani wa gari hilo la kifahari ambalo hata hivyo lilikutwa kifaa cha kufuatilia mwenendo wa gari (Car Track) kikiwa kimeharibiwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah akizungka kutizma hilo gari nje ya kituo kikuu cha Polisi mjini Moshi .
Post A Comment: