Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amepiga marufuku kwa hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini kuonesha muziki katika maeneo yote yakutolea huduma na kuwataka kuweka jumbe zinazohusu Elimu Afya kwa umma pindi wanapongoja kupata huduma.

Ameyasema hayo mapema leo wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika ukumbi wa halmashauri ya Muleba katika Mkoa wa Kagera."Ni marufuku kwa hospital zote kuonesha miziki katika maeneo yote ya utoaji huduma za afya" alisema Dkt Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile amemwagiza Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara DKt. Revokatus Ndyekobora kuhamasisha wananchi Juu ya umuhimu wa kuudhuria kliniki kwa mama mjamzito walau mara nne ndani ya kipindi chá ujauzito wake na kuhakikisha wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

"Tuongeze kasi katika kuhamasisha wakina mama wajawazito kuhudhuria kliniki, na kwenda kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya" alisema Dkt Ndugulile. Pia alisema kuwa Serikali inaendelea kuboresha sekta ya Áfya nchini kwa kutoa pesa ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya na kuhamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi wa vituo hivyo (Forced account)

"miundombinu tunaendelea kuboresha, Mkoa mzima tumeleta shilingi Bilion 5.9 kwaajili ya kuboresha vituo vya Áfya, viwili vikiwa katika Wilaya ya Ngara "alisema Dkt Ndugulile .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: