Ahmad Mmow, Lindi
NAIBU waziri wa maji na umwagiliaji Juma Àweso amemsimamisha kazi mkandarasi anae jenga mradi wa maji wa Ng'apa uliopo katika manispaa ya Lindi kwa kushindwa kumaliza kwa wakati.
Uweso amesikitishwa na kitendo cha mkandarasi wa kampuni ya OVERSEAS INFRASTRUCTURE ALLIANCE, baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo alisema ameamua kumsimamisha mkandarasi huyo kutokana na kushindwa kumaliza mradi huo wa maji wa Ng’apa tangu ulipoanza mwaka 2013.
Naibu waziri Aweso alisema ameamua kumsimamisha kazi mkandarasi huyo kutokana na kushindwa kumaliza mradi huo kwa wakati licha ya kufika viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Rais John Magufuli ambapo mradi huo ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2013 na ulitakiwa kumalizika mwaka 2015 lakini hadi sasa mradi haujakamilika licha ya kufikia asilimia 90 .
Naibu waziri huyo aliendelea kusema kuwa hakuna sababu za msingi za kushindwa mradi usimalizike kwa wakati unaotakiwa pamoja kuwepo fedha za mradi huo shs.bil.13
Naibu waziri Aweso alikataa kuendelea kukagua mradi huo akiweka wazi ujanja ujanja wa mkandarasi ulishindwa kumshawishi aendelee kukagua mradi huo.
Kwa upande wake mhandisi mshauri mkazi wa mradi huo kutoka kampuni ya G.K.W Consult kutoka nchini Ujeruman Mhandisi Audax Rweymam, alishashauri kuwa mkandarasi huyo asimamishwe na wataalamu kutoka wizarani waje kusimamia nakumalizia kazi iliyobaki( asilimia hiyo kumi iliyobaki)
Nae kaimu mkuu wa mkoa Lindi ambae ni mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga alieleza juhudi za mkoa kusukuma mradi huo ukamikike kwa wakati na kushugulikia changamoto mbalimbali. Hata hivyo bado juhudi hizo hazikufua dafu na umeshindwa kumalizika kwa wakati.
Mradi huo ni miongoni mwa miradi ambayo imetembelewa na kutolewa na maagizo na viongozi wakuu wa kitaifa.Wakiwao Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania,Dkt John Magufulia waziri mkuu,Kassim Majaliwa.
Post A Comment: