Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi NACTE limesema tayari limetunga  kanuni na taratibu mpya ambazo zitadhibiti usajili na uendeshaji wa vyuo hapa nchini lengo likiwa ni kupunguza utitiri wa vyuo ambavyo vipo lakini badala ya kuweka mbele ubora wa elimu vimebaki kukimbizana kufanya biashara.

Naye Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amealitaka baraza hilo kuvifungia vyuo vyote vinavyotoea huduma chini ya kiwango na hata kama kitakuwa ni chuo cha serikali.

Profesa John Kondoro ni Mwenyekiti wa Baraza la uongozi la NACTE ambaye anasema watasimamia sheria na kuhakisha vyuo vinatekeleza majukumu yake kwa misingi na sheria zilizopo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: