Aliyekuwa mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara amesema kwa hali ilivyo ya kisiasa katika jimbo hilo tayari ameshinda.
Waitara anasema anajiandaa kuendelea kuwatumikia wana Ukonga baada ya uchaguzi wa Septemba 16, 2018 kumshinda mgombea wa Chadema, Asia Msangi.
“Mimi ni mbunge ninayeendelea na ninapozungumza na wananchi nasema ninafanya lakini mgombea mwenzangu wa Chadema (Asia Msangi) anasema nitafanya, sasa huoni nimekwisha shinda,” Waitara amelieleza gazeti la Mwananchi.
Amesema kampeni zake atazizindua rasmi Septemba mosi na kwa sasa anafanya mikutano ya chini kwa chini kwa kukutana na makundi mbalimbali kuzungumza nayo.
Waitara aliyewahi kuwa CCM akahamia Chadema na kurudio tena CCM Julai 28, ameanika mbinu zake sita zitakazomwezesha kumshinda Asia.
Amezitaja mbinu hizo kuwa ni mikutano ya hadhara; kukutana na makundi mbalimbali kama bodaboda; wafanyabiashara; vikoba na kutembea mtaa kwa mtaa.
“Mbinu ya nne ni kutoa mrejesho wa miradi niliyoifanya, tano; kuonyesha kero zilizopo na mwisho namna tutakavyozishughulikia,” amesema Waitara
Post A Comment: