Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Mhe. Zebedayo Athuman hivi leo amekutana na halmashauri kuu maalum ya kata ya Pamba wakiwemo wajumbe halmashauri kuu, viongozi wa madhehebu ya dini, wazee maarufu pamoja na watendaji wa serikali, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi katika kata zote 18. Pamoja na utoaji wa Bendera na vitendea kazi kila tawi.

Mhe. Zebedayo akizungumza na halmashauri kuu maalumu ya Kata, ameto shukurani za dhati kwa Wana CCM kumwamini na  kumchagua katika uchaguzi uliopita ameahidi kuwatumikia kwa uadirifu na ubunifu ili kuleta uhai wa chama na kuimarisha uchumi. Kadharika amewaasa wana CCM  kuvunja makundi yasiyonatija katika mstakabali wa ujenzi wa chama. Ameasa viongozi wa kata na matawi  kufuata katiba na kanuni mbalimbali katika uendeshaji wa Chama, ikiwepo uzingatiaji wa Vikao vyote vilivyoainishwa kwa mujibu wa katiba.

Mhe. Zebedayo amewaasa wana CCM kujipanga kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020,  ikiwa ni pamoja na kuweka mkakati wa kulinda mitaa yote inayomilikiwa na CCM na kukomboa mitaa mitatu iliyopo upinzani. Uongozi wa Kata kuwalipa posho Mabalozi na watendaji wote wa matawi kwa wakati pamoja na kufuata utaratibu wa TEHAMA kwa mapato na matumizi. Mhe Zebedayo akijibu taarifa ya Chama na maoni ya wajumbe wa kikao amesema ataunda kamati ndogo ya maadili kuja kuchunguza na kusaidia kutatua migogoro ya kichama.

Naye katibu wa CCM Nyamagana Ndg. Salum Kalli akimkaribisha Mwenyekiti Mhe Zebedayo, ametumia adhira hiyo kujitambulisha, nakusema anaudhoefu wa kutosha kufanikisha uchaguzi na atakuwa tayari kuutumia udhoefu huo kulejesha mitaa 72 iliyopo upinzani.

Naye mwenezi wa CCM Wilaya Ndg. Mustapha Banigwa pamoja na Zamda Kamgisha wamewaasa viongozi wa Kata na matawi kutoa taarifa za fedha katika kamati ya siasa na kufikisha maombi ya matumizi ya fedha mwezi mmoja kabla kwa tarehe 21-24 ya mwezi.

Akisoma taarifa ya Chama kwa Mwenyikiti, Ndg Agustine Bwire amesema kunakusua ongezeko la wanachama kutokana na dhana ya wanachama kusubiri hisani ya wagombea kununuliwa na kulipiwa kadi, makundi ya kisiasa kushamimili kwa fukuta uchaguzi.

Naye Mwenyekiti wa Kata ya Pamba Ayubu Oyugi akihairisha kikao hicho amesema Kata ya Pamba imegubikwa na makundi, hivyo wapotayari kupokea kamati maalum kama mwenyekiti alivyopendekeza ili kusaidia kuvunja makundi hayo.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: