Na Frankius
Cleophace Tarime.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara Samwel Kiboye No3 amewataka wananchi
Wilayani Tarime Mkoani Mara kudumisha amani katika Uchaguzi mdogo wa kata ya
Turwa Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Mwenyekiti
huyo amesema hayo baada ya Mkutano wa kampeni jana uliofanyika katika Viwanja
vya Soko la Rebu Mjini Tarime ambao umeudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo
Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku (Msukuma) , na aliyekuwa Mbunge
wa Jimbo la ukonga Mwita Waitara ambaye kwa sasa amejiunga na Chama cha Mapinduzi.
Kiboye
amesema kuwa wao kama viongozi hawatakubali Wananchi kufanya fujo bila kujalai
itikadi za vyama bali wananchi hao waende kupiga kura na kisha kuondoka
Nyumbani kwa ajili ya kusubili Matokeo.
“Tumewakataza
Vijana wa CCM Wasifanye fujo hivyo hatutafumbia Macho pia Vijana wa Vyama vya
Upinzani watakaofanyafujo lazima amani itawale Tarime Uchaguzi ufanyike kwa
amani” alisema Kiboye.
Samweli
ameongeza kuwa wananchi wamchangue mgombea anayetokana na CCM Mwita Ghati kwa
sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anachapa Kazi kwani Diwani huyo
atafanyakazi bila kujali itikadi za vyama kama Rais wa Tanzania anavyofanya
kazi kwa watanzania wote bila kujali waliomchagua na ambao hawakumchagua.
Kwa upande
wake Mwita Waitara ambaye alikuwa Mbunge wa Ukongo kupitia CHADEMA amesema kuwa
ameamua kwenda CCM bila kushikinikizwa
na Mtu yeyote badala ya Chama chake kushindwa kusiliza Mapendekezo yake huku akidai kuwashughulikia Viongozi
wanatokana na CHADEMA kuanzia ngazi ya taifa hadi tawi wakiwemo Wabunge wa
Upinzani.
Aidha Mbunge
wa Geita Mjini Joseph Kasheku (Msukuma) amesem akuwa watanzania walikuwa
wanataka Mabadiliko pamoja na huduma za kijamii assa zimefanyika na zinaendelea
kufanyika kwa kasi hivyo amewataka
Wanachama Wapinzania kurudi CCM.
Uchaguzi
mdogo wa Turwa unatarajia kufanyika Agost 12 Mwaka huu baada ya aliyekuwa
diwani wa kataya Turwa CHADEMA Zakayo Chacha Wangwe kujiunga na Chama Cha
Mapinduzi CCM.
Post A Comment: