Mkimbiza Mwenge Kitaifa  Mhandisi Charles Francis Kabeo amefungua shule ya Msingi Buhongwa B iliyogharimu shilingi 182,249,250.00.

Mhe. Mhandishi Kabeo akifungua shule hiyo amepongeza uongozi wa Wilaya ya Nyamagana ukisimamiwa na Mkuu wa Wilaya Dkt Philp Nyimbi, Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula pamoja baraza la madiwani  na watendaji wote wa halmshauri ya Jiji la Mwanza hususani uongozi wa shule kwa usimamizi wa ujenzi wa shule ubora na ya mfano iliyozingatia thamani ya fedha. Ambapo viongozi Hao walipewa heshima ya kushika Mwenge wa Uhuru kwa kazi nzuri.

*Nimeridhika na nifaraja kuona ujenzi unazingatia ubora na thamani halisi ya fedha hakika hii ni shule ya mfano* Mhandisi Kabeo amesema.

Shule ya Buhongwa B iliyopo kata ya Buhongwa wilayani  Nyamagana imegharimu shilingi 182,249,250.00. Gharama hizo zikiwa fedha kutoka serikali kuu 57,300,00.00 ambapo halmashauri ya Jiji la Mwanza ikichangia shilingi 89,468,250.00 na mchango wa jamii pamoja na nguvu kazi ikiwa ni 35,481,000.00.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿




Share To:

msumbanews

Post A Comment: