Joseph Ngilisho
,Arusha
Wataalamu wa manunuzi
ya Umma nchini wametakiwa kuzingatia weredi katika
utendaji wao wa kazi na kuepukana
na vitendo vya ubadhilifu ,rushwa na
matumizi mabaya ya fedha za umma jambo litakalosaidia kudhibiti matumizi mabaya
ya fedha na kusaidia fedha hizo kutumika katika maendeleo mapana zaidi
ya Taifa.
Akiongea kwa niaba ya
Rais John Magufuli,wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku tatu wa wataalamu
na wabobezi wa manunuzi ya umma(IPPC) kutoka nchini 46 duniani unaofanyika jijini
Arusha,nchini Tanzania,waziri wa fedha na mipango dkt.Philp Mpango amesema
mkutano huo unalenga kujadiliana namna
ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia taknolojia mpya ya
manunuzi .
‘’Ununuzi wa umma ndio
sehemu kubwa ambapo fedha za bajeti zinapita
hivyo ukifanyika vibaya maana yake serikali inapata hasara ndio maana
tunasisitiza weredi wa wataalamu wa manunuzi kwa sababu kuna mamunuzi hewa na
miradi hewa ’amesema dkt Mpango
Aidha amesema asilimia
70 ya fedha za matumizi ya kawaida zinapitia ununuzi wa umma na asilimia 100 ya
bajeti ya fedha zote za maendeleo
zinapitia manunuzi ya umma ,hivyo bajeti zote katika maeneo hayo mawili
zikitumika vibaya lazima serikali iumie.
Amesema wataalamu wa
manunuzi ya Umma wakitumia vizuri taaluma yao itasaidia maeneo mengine ya sera
katika kukuza viwanda na kuinua sekta binafsi hivyo ununuzi utumike vizuri ili
kusaidia kuinua nchi za afrika ikiwemo Tanzania kuendana na teknolojia iliyopo.
Awali Mwenyekiti wa
bodi ya manunuzi ya umma nchini,dkt Hellen Bandiho amesema taasisi yao imeanza kuchukua hatua kwa
wataalamu wake wasiozingatia weredi na maadili katika kazi zao na kuwataka
waajiri kuhakikisha wanachukua wataalamu
wa manunuzi ya umma wenye usajiri wa bodi yao.
‘’Wataalamu wa
manunuzi ya umma wasio na usajiri ambalo wameajiriwa ama kufanya kazi zao bila
usajiri ni makosa kwao na kwa mwajiri aliyewaajiri na hatua kali zitachukuliwa’’Amesema
dkt Bandiho
Alivitaka vyombo vya
dola kama polisi,takukuru na mahakama kushirikiana katika kuwaibuka na
kuwachukulia hatua watu hao ambao wamekuwa wakiipaka matope bodi hiyo kwa
kuendesha shughuli zako kinyume cha sheria.
Post A Comment: