Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Tudeley Estates Ltd, Jensen Natal na Mwanasheria wa kampuni hiyo, Edward Mroso kwa tuhuma za kukwepa kodi ya serikali kiasi cha zaidi ya  sh. milioni 800 .

Pia ameiamuru Idara ya Uhamiaji Wilayani humo kumnyang'anya hati ya kusafiria meneja wa kampuni hiyo, Trevor Gifford hadi fedha hizo zitakapolipwa.

Kampuni ya Tudeley inamiliki na kuendesha mashamba ya ushirika ya chama cha msingi cha Murososangi yenye ukubwa wa ekari 2,054.

Ole Sabaya, ametoa maagizo hayo jana Agosti 16 wakati alipofanya ziara ya kutembelea mashamba ya kampuni hiyo huku akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Hai.

Pia aliambatana na Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wilayani Hai, Spécioza Owere.

Kabla ya kuingia katika lango kuu la kampuni hiyo Ole Sabaya aliamuru Gifford aitwe huku akiwa na hati yake ya kusafiria na  baadaye akaingia katika ofisi za kampuni hiyo.

Akizungumza katika eneo la tukio, Ole Sabaya alisema kwamba ana taarifa za  uhakika kwamba kampuni hiyo imekuwa ikikwepa kulipa kodi ya serikali kwa muda wa miaka saba hadi sasa.

Ole Sabaya alisema kwamba kampuni hiyo imekwepa kulipa kodi ya serikali zaidi ya Sh800 milioni ambazo ni malimbikizo ya kodi ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Akitoa maagizo hayo Ole Sabaya aliliamuru jeshi la polisi Wilayani humo kumkamata Natal  na Mroso na kuwekwa mahabusu  kwa saa 48 na wahakikishe fedha hizo ambazo ni kodi ya serikali zinalipwa.

"Wewe utaenda ndani ili uje uniambie kuna utaratibu gani wa kodi ya serikali kulipwa na ijumaa asubuhi uwepo ofisini kwangu uniambie kodi ya serikali italipwaje,” alisema  na kuongeza:

"Chukua passport yake ya zamani na sasa nataka pésa hiyo ilipwe ndani ya siku saba na TRA niletewe maelezo hayo.”

Mara baada ya agizo hilo maofisa wa jeshi jeshi la Polisi Wilayani humo walimkamata Natal na Mroso na kisha kuwapéleka kwenye gari huku maofisa wa idara ya Uhamiaji wakichukua hati ya kusafiria ya Trevor.

Kabla ya Mroso kushikiliwa alimweleza Ole Sabaya kwamba uongozi wa kampuni hiyo ulishawasilisha maombi mbele ya ofisi yake kuwaomba TRA wakague hesabu na madeni ili waweze kulipa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: