Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza kwa mara ya kwanza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya Hai katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Baadhi ya Watumishi katika Halmashauri ya Hai wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya hiyo alipozungumza nao kwa mara ya kwanza.Baadhi ya Madiwani wakiwa katika kikao cha kwanza na Mkuu wa wilaya ya Hai na watumishi wa Halmashauri hiyo. Katibu Tawala wa wilaa ya Hai,Upendo Wela akizungumza katika kikao hicho.Baaadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai. Baaadhi ya Wakuu wa Idara a Halmashauri hiyo. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,waichangia jambo katika kutano wa Mkuu wa wilaya ya Hai na Watumishi wa Halmashauri hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
MKUU mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya amekemea vikali vitendo vya Rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo hali iliyopelekea kutajwa kama mteja namba moja wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa( TAKUKURU) katika mkoa wa Kilimanjaro.
Sabaya pia ameinyooshea kidole idara ya Ushirika katika Halmashauri hiyo ambayo inatajwa kushindwa kusimamia vyama vya ushirika hadi kupelekea kuingia mikataba aliyoitaja kuwa ya hovyo na yenye kujaa rushwa.
Katika kikao chake na watumishi wa Halmashauri ya wilaya kilicholenga kujitamburisha kwa watumishi hao Sabaya alisema Halmashauri hiyo inaongoza kwa ubadhilifu wa mali za umma na kwamba hadi sasa amepata taarifa za uwepo wa kesi nane zinazohusu rushwa.
“Mnaongoza kwa ubadhilifu na wa mali za umma,naambiwa kuna kesi nyingine zinaendelea na Takukuru inachunguza nyingine , hii ni aibu na ni fedheha kwa Halmashauri ,kama una mikono michafu hauna uhalali wa kumuubiri mtu habari njema niwaombe mbadilike”alisema Ole Sabaya.
Mkuu huyo wa wilaya alisema zipo taarifa ya kuwa katika Halmashauri hiyo kuna baadhi ya watu wamejijengea tabia ya kutaka kuonekana kama miungu watu kwa kufanya maamuzi bal ya kuwashirikisha watu wengine huku akimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Yohana Sintoo kulitazama hilo.
“Nimesikia wapo watu hapa ,wao mnakaa kwenye CMT(kikaocha ushauri ) mnafanya maamuzi yeye ni mungu mtu hapa ,ikifika wakati wa kutekeleza hawatekelezi ,mnawakatisha tamaa watumishi wengine walioko tayari kufany kazi ,walioko tayari kutekeleza yale tuliyoahidi wananchi tunategemea hao watu wabadilike”alisema Ole Sabaya.
“Kwa hiyo nategemea sana kwenye eneo la rushwa tuwe na mabadiliko makubwa ,lakini nikupongeze Mkurugenzi ,nilikuwa napitia taarifa ya CAG ya mwaka 2014 kwenda 2015 kulikuwa na hoja 83 leo amezishusha hadi kufikia hoja 6 jambo la kupongezwa lakini hata hizo sita ziondoke.”aliongeza Ole Sabaya.
Kuhusu Ushirika ,Ole Sabaya alisema katika mambo ambayo Halmashauri hiyo imeanguka ni eneo la ushirika huku akiitaka idara ya ushirika kwa kushirikiana na ofisi ya Mwanasheria wa Halmashauri hiyo kupiia mikata iliyoingiwa kati ya Vyama vya Ushirika na wawekezaji.
“Kati ya sehemu tumefeli na tuna aibu kubwa ni eneo la Ushirika, kuna mikataba ya ajabu ajabu sijawahi kuona lakini mingine ni ninyi wenyewe mmeshindwa kutimiza wajibu wenu ,ukiangalia vile vyama vya ushirika na mikataba waliyoingia na wale wawekezaji na fedha wanazo zipata ,hata pengine kodi za serikali mmeikwepa kwa miaka mingi “alisema Ole Sabaya.
Alisema endapo Idara ya Ushirika ingetekeleza vyema wajibu wake leo hii kuisngekuwa kuwa na kilio cha mapato kwenye Halmashauri hiy kwani ingewawezesha kupata hata asilimia 2 kwenye mapato ya Vyama vya ushirika .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo alikiri kuwepo kwa vitendo vya watumishi wa halmashauri hiyo kujihusisha na masuala ya rushwa na kupelekea kutajwa kama mteja mkuu wa TAKUKURU.
“Halmashauri ya wilaya ya Hai ilikuwa ni mteja Mkuu wa Takukuru,kwa maana ya kwamba idadi ya kesi na watu waliopelekewa kule ,kwa muda wa miaka miwli sasa tangu nifike hapa na nilijisikia uchungu kidogo siku moja tukiwa kwenye zoezi la mwenge ,afisa mmoja wa Takukuru alipoulizwa mteja wako mkuu ni nani alisema ni halmashauri ya wilaya ya hai”alisema Sintoo.
Alisema hali hiyo ilimpa wakati mgumu na kuamua kutengeneza miakakati ya kuhakikisha anaondoa hali ya kuwa mteja wa Takukuru na tayari matokeo yameana kuonekana ambapo katika kipindi cha miaka tangu aingine hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa na kupelekwa mahakamani .
Kwenye eneo la ushirika ,Mkurugenzi huyo alisema ni kweli kuna changamoto iliyotokana na sheria ya ushirika inayotajwa kutoa mwanya katika eneo la uongozi kuendelea kukaa madarakani kwa kipindi kirefu bila ya kuwa na ukomo.
“Sheria ya ushirika ilikuwa inatoa mwanya na nina imani imeendelea kufanyiwa kazi katika eneo la ukomo wa uongozi imekuwa ni changamoto kubwa sana kuna wenyeviti wanaoongoza hizi Amcos na maeneo ya ushirika bila ya ukomo “alisema Sintoo.
“Unakuta mtu tangia mwaka 70,80 hadi 90 yeye ni kiongozi tu unaweza kuona kuna changamoto ya aina yake .yule yule, yule na anafanya makosa na kwa kuwa amekaa muda mrefu amezoeana na watu na hivyo ni vigumu kuchukuliwa hatua .”aliongeza Sintoo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya ameanza kukutana na makundi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya hiyo kwa kuanza na watumishi ambapo anataraji pia kuzungumza na wazee na viongozi wa dini katika halmashauri hiyo.
Post A Comment: