Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Internews Tanzania wameendesha mafunzo kwa waandishi wa Habari Kanda ya Kaskazini/Magharibi (Geita, Shinyanga na Simiyu) kuhusu Changamoto za Sheria mpya za habari.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Agosti 17,2018 hadi Agosti 18,2018 yanafanyika katika ukumbi wa Alpha Hotel Mjini Geita.
Akifungua Mafunzo hayo,Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa alisema kupitia mafunzo hayo waandishi wa habari watajengewa uelewa kiuhusu sheria mbalimbali zinazohusu vyombo vya habari na waandishi wa habari na namna waandishi wa habari wanavyoweza kuishi na sheria hizo.
"Lengo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari na kuangalia changamoto zinazotolewa na sheria hizi sambasamba na kukumbushana miiko ya uandishi wa habari lakini pia kufahamu nafasi ya mwandishi wa habari kama mtetezi wa haki za binadamu",alisema.
Naye Afisa Mradi wa Boresha Habari kupitia Shirika la Internews linalofadhiliwa na USAID Victoria Rowan aliwasihi waandishi wa habari waliopata fursa ya kushiriki mafunzo hayo kutumia vyema elimu wanayopewa.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari mikoa ya Geita Shinyanga na Simiyu kuhusu Sheria za vyombo vya habari katika ukumbi wa Alpha Hotel Mjini Geita - Picha zote na Kadama Malunde & Joel Maduka
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akielezea malengo ya semina hiyo
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa
Afisa Mradi wa Boresha Habari kupitia Shirika la Internews Victoria Rowan akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Afisa Mradi wa Boresha Habari kupitia Shirika la Internews Victoria Rowan akielezea jambo ukumbini
Mwezeshaji katika Mafunzo hayo,Wakili James Marenga akitoa mada kuhusu Sheria ya Huduma za Habari
Mwezeshaji katika Mafunzo hayo,Wakili James Marenga akifafanua vifungu mbalimbali vya sheria
Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde1 blog akifuatilia mada ukumbini.Kulia ni Bahati Sonda kutoka mkoani Simiyu
Mwandishi wa habari Salma Mrisho kutoka Geita akichangia mada
Mwandishi wa habari Paschal Michael kutoka mkoa wa Simiyu akichangia hoja ukumbini
Mwandishi wa habari Rehema Matowo kutoka Geita akichangia mada
Semina inaendelea
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Kushoto ni Mwandishi wa habari Rose Mweko kutoka mkoani Geita akiwa na Derick Milton kutoka Simiyu na Editha Edward kutoka Geita
Washiriki wakifuatialia mada ukumbini
Semina inaendelea
Washiriki wakifuatilia mada
Mafunzo yanaendelea
Mwandishi wa habari Joel Maduka (kulia) kutoka Geita na Bahati Sonda kutoka Simiyu wakiwa ukumbini
Mwandishi wa habari Stella Ibengwe kutoka Shinyanga akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo
Mwandishi wa Habari Rehema Evance kutoka Simiyu akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo
Mwandishi wa habari Osman Nyamiti kutoka Divine Fm Shinyanga akichangia mada ukumbini
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Geita, Daniel Limbe akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Post A Comment: