Mgonjwa aliyekuwa akisafirishwa na gari la kubebea wagonjwa (AMBULANCE) amepoteza maisha na watatu kujeruhiwa baada ya gari yenye namba ya usajiri DFPA 3273 kupinduka kata ya Ilembo Manispaa ya Mpanda mkoani katavi wakati gari hilo likitokea Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kumpeleka mgonjwa Rufaa Jijini Mbeya.

Gari hiyo yenye nomba za usajili DFPA 3273 Mali ya Hospitali ya Manispaa ya Mpanda ilikuwa ikielekea Mbeya ikimsafirisha Mgonjwa ambae ni Mtoto Hollo Balida mwenye miaka 10 ambae amefariki hapo hapo baada ya ajali hiyo kama anavyoeleza mama mzazi wa Marehemu.

Kwa upande wake wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Obed Mahenge amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alikuwa na haya ya kusema.

Kutokana na ajri tatu mfururizo zilizotokea katika halamshauri ya Manispaa ya Mpanda nimeweza kuzungumza na baadhi ya madreva alikuwa na haya ya kusema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: