Mfanyabiashara Davis Mosha
alikamatwa Agosti Mosi, 2018 kwa madai ya kuwazuia askari wa Idara ya
Uhamiaji kutekeleza majukumu yao na bado anaendelea kushikiliwa kwa
hatua zaidi.
Msemaji
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda amesema Mosha aliwashambulia
askari hao na kumnyang’anya mmoja wao simu ya mkononi baada ya kufika
katika jengo la Delina lililopo Sinza Mori.
“Askari walifika kwenye majengo hayo na kujitambulisha kwa mlinzi na moja kwa moja walionyeshwa ofisi za meneja.
"Wakati
wakifanya mazungumzo ya kikazi na meneja huyo, ghafla akatokea Mosha na
kuanza kuwafokea, kisha kuwashambulia na kumnyang’anya askari mmoja
simu yake.” –Mtanda
Amesema
alichofanya Mosha ni kinyume cha sheria ya uhamiaji namba 54 kifungu
cha 45 kipengele 1 F, kinachozungumzia kumzuia ofisa wa uhamiaji kufanya
kazi yake ya ukaguzi.
Mtanda amesema bado wanamshikilia Mosha kwa uchunguzi zaidi na kama kuna hatua nyingine zitafuata watatoa taarifa.
Mtanda amesema bado wanamshikilia Mosha kwa uchunguzi zaidi na kama kuna hatua nyingine zitafuata watatoa taarifa.
Post A Comment: