Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula kwa ushirikianao na taasis ya First Community Organisation hivi leo amekabidhi vifaa vya michezo na Jezi kwa vikosi 9 vinavyoshiriki  ungwe ya pili ya michuano ya kombe la NDFA"Nyamagana District Football Association" kwa mwaka 2018 hadi 2020.

Mwenyekiti wa taasis ya First Community Ndg. Ahmed Misanga akizungunza kwa niaba ya Mhe. Stanislaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana, amefafanua vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na vifaa vya michezo Jezi kwa vikosi 9, Mipira 5 zenye thaamani ya shilingi 4,200,000. Ndg. Misanga amesema Mhe. Mabula  yupo tayari kuinua michezo Nyamagana kwakuwa michezo ni afya na ajira.

Udhamini huo utadumu kwa miaka mitatu 2018-2020 mfululizo utahusisha utoaji wa zawadi kwa washindi wa michuano hiyo, ikiwa mshindi wa kwanza mwaka 2018 atajinyakulia Kombe na kitita cha Tsh 500,000 tslimu,  mshindi wa pili atapata Kombe na fedha taslimu Tsh 200,000, Mipira Miwili, Mfungaji Bora atapatiwa, Golden boot na fedha taslimu shilingi 50,000/, mwamuzi bora atapata kisanduku cha vifaa na fedha taslimu  50,000, na kila mwaka  zawadi zitaongezwa pamoja na kuboreshwa kulingana na mahitaji ya wakati.

Ndg.Kurwijila Malima akiongea kwaniaba ya MZFA "Mwanza Football Association" amepongeza Mhe. Mabula kwa jitihada zake kudhamini michuano  ngazi ya wilaya, maana wadhamamini wengi wamekuwa wakifadhiri michuano ya kimkoa na kitaifa.

Naye katibu wa NDFA Ndg. Domicianus Valenco Amesema michuano hii imefikia ungwe ya pili itakayozihusisha vikosi bora 9 katika vikosi 27 vilivyoshiriki ungwe ya kwanza ambapo mshindi wa kwanza na pili watarnda katika michuano ya Mkoa wa Mwanza. Amchukua fursa hiyo kumpongeza Mhe. Mabula kwa udhamini wake ambao ni chachu na hamasa na michuano hiyo.

Mwenyekiti wa Kikosi cha Wajasiri FC Ndg. William Silvester akizungumza kwa niaba ya vikosi vishiriki  amemshukuru Mhe. Mabula kwa udhamini huo ambao umefika wakati muafaka wakiwa wanauhitaji wa jezi na vitendea kazi.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: