Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula, ameendelea na utaratibu wa kupokea na kusikiliza kero pamoja na changamoto za wananchi kupitia makundi maaulum. Akiwa ameambatana na Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Nyamagana Ndg Mustapha Banigwa, wametembelea Kijiwe cha Kahawa Buhongwa kwa Roja, ambapo wananchi walipata fursa ya kuzungumza na Mbunge kuhusiana na changamoto zinazowakabili ikiwemo miundombinu ya barabara, Maji, Afya pamoja na ajira kwa Vijana.

Mhe Mabula akijibu hoja ya ajira, amewasihi Vijana na Wanawake kujiunga na Vikundi vya ujasirimali Kilimo, Uchuuzi, Mama lishe, ufugaji au Uvuvi kulingana na biashara walizonazo. Kisha ofisi yake ipo tayari kugharamia mafunzo ya ujasirimali na uandikaji miradi, biashara na masoko, uandaaji wa katiba na usajiri kwa vikundi ambavyo havijasajiliwa. Ili kunufaika na 10% ya mapato ya halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Naye mmiliki wa kijiwe hicho cha Kahawa Roja amempongeza Mbunge kwa utaratibu wa kuwafikia wafanyabiashara ndogo ndogo maeneo yao ya kazi maana ndio taswira ya uongozi bora.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: