Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula hivi Leo ameendelea na ziara ya ukaguzi wa Miradi ya maendeleo Kata ya Isamiro ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika kata 18 za halmashauri ya Jiji la Mwanza. Ambapo leo amekagua ujenzi wa barabara ya mawe inayoziunganisha Kata mbili ya Isamiro kuelekea kata ya Mbugani Nyanshana, barabara yenye urefu wa kilometa 1.2.
Mhe Mabula ameipongeza serikali ya CCM inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteleza Ilani ya Uchaguzi kwa vitendo Jimbo la Nyamagana. Mhe Mabula amebainisha hayo alipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo Kata ya Isamiro kuelekea kata ya Mbugani kwenye mkutano wa hadhara.
"Ninafarajika kuona tunatekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara ya Mawe ya Dkt Migoro kuelekea Nyashana itakayo gharimu shilingi Bil 1.1 na kuwa mkombozi kwa wananchi wa kata hizi mbili hususani waishio maeneo ya miinuko". Mhe Mabula amesema
Mhe Mabula amesema kata ya Isamiro imejengewa barabara mbili moja ikiwa ya kiwango cha rami yenye urefu wa kilometer 0.6 sanjari na hii ya mawe yenye urefu wa kilometers 1.2 itakayogharimu shilingi billion 1.1 na katika mwaka huu wa fedha serikali imetoa shilingi 700,000,000 kwaajili ya kuendelea na kazi.
Mhe Mabula ameambana na mwenyeji wake Charlse Nyamasiriri Diwani Kata ya Isamiro, Katibu hamasa na Chipukizi Hussein Kimu pamoja na watendaji wa serikali.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana 🇹🇿
Post A Comment: