Mbunge
wa Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu, akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Makungu waliokuwa na mabango yenye ujumbe wa kero
mbalimbali walipo usimamisha msafara wake wakati akipita kijijini hapo
akienda kuhutubia mkutano wa hadhara Kata ya Iyumbu wilayani Ikungi
mkoani humo jana.
Mheshimiwa Kingu akisisitiza jambo kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Iyumbu.
Mheshimiwa Kingu akicheza sanjari na wasanii wa Kikundi cha Iwambala cha kata hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
wasanii wa Kikundi cha Iwambala cha kata hiyo wakiburudisha.
Mheshimiwa Kingu akiwatuza wasanii hao.
Muonekana
wa meza kuu kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa
Kata ya Iyumbu, Mohamed Athumani, Diwani wa Kata hiyo, Peter Gwiligwa,
Mbunge wa jimbo hilo, Elibariki Kingu na Mwenyekiti wa Kata ya Iyumbu,
Boniphace Gwanda.
Diwani wa Kata ya Iyumbu, Peter Gwiligwa akizungumza kwenye mkutano huo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE
wa Singida Magharibi Mhemiwa, Elibariki Kingu alilazimika kutoa
machozi baada ya wananchi wa Kijiji cha Makungu kilicho katika
Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi kumpokea kwa mabango yenye ujumbe wa kero
mbalimbali ambazo alianza kuzifanyia kazi lakini watendaji kushindwa
kuzisimamia.
Wananchi
hao waliokuwa na jaziba waliusimamisha msafara wake kijiji hapo jana
wakati akielekea Kata ya Iyumbu kufanya mkutano wa hadhara ambapo
walikuwa na mabango yaliyo kuwa yakielezea changamoto mbalimbali
walizonazo.
Changamoto
kubwa walizoziandika kwenye mabango hayo ni kutokuwa na shule, maji,
zahanati na barabara ya uhakika ambapo walimtaka mbunge awape majibu ya
kero hizo.
Akizungumza
na wananchi hao Kingu alisema baada ya kuchaguliwa alitoa mifuko ya
saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa zahanati, Shule ya Msingi Makungu
pamoja na fedha sh.milioni 70 kwa ajili ya mradi wa maji na kilicho
hitajika ni nguvu ya wananchi kuendeleza miradi hiyo.
Baada
ya mbunge huyo kutoa maelezo hayo ndipo ilipobainika kuwa saruji
iliyotolewa na mbunge huyo tangu mwaka 2016 kwa ajili ya miradi hiyo
bado ilikuwa imefungiwa ndani na watendaji wa kijiji hicho bila
kuifanyia kazi huku cheki ya sh.600,000 iliyotolewa na Halmshauri ya
Wilaya ya Ikungi kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo kwenye
kijiji hicho ikipoteza muda wake bila ya fedha kutolewa benki.
"Wananchi
wangu mmesikia wenyewe jinsi nilivyo jitahidi kusaidia katika ujenzi wa
zahanati na shule kwa kuwaletea saruji sasa hapo mwenye kosa ni nani
mimi au watendaji wenu waliofungia saruji ndani kwa muda wote huo bila
ya kuzifanyia kazi" alihoji Kingu.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Iyumbu, Kingu aliwataka
watendaji hao kufanya kazi badala ya kuwa mzigo kwa wananchi huku
akisema ni lazima ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) itekelezwe kwa
vitendo kwa kuwaletea maendeleo wananchi na si vinginevyo.
Kingu
aliwaambia viongozi hao kuwa wawe na huruma kwa wananchi kutokana na
ukubwa wa jimbo hilo kwani kutoka makao makuu ya wilaya hadi katika kata
hiyo ambayo ipo mpakani mwa mkoa wa Singida na Tabora ni kilometa 240
ni sawa kutoka Morogoro hadi Dodoma hivyo wasikubali kupoteza bure nguvu
za maendeleo kwa ajili ya wananchi kutokana na vifaa vingi vya ujenzi
kusafirishwa kwa umbali huo na wao kuvitelekeza bila ya kuvifanyia kazi.
Katika
mkutano huo mambo mengi yalijitokeza na sababu ya kukwama kwa miradi
hiyo ya maendeleo kuwa kumechangiwa na watendaji wa vijiji na viongozi
wa siasa kusigana kwa kuingiliana majukumu yao ya kazi huku diwani wa
kata hiyo akishindwa kusimamia miradi hiyo.
Mkutano
huo ulikwisha kwa kutiliana saini mkataba wa kumaliza miradi hiyo
ambapo Kingu aliahidi kwenda katika kata hiyo kupiga kambi ya siku 10
ili kuhakikisha miradi hiyo inaanza upya kufanyiwa kazi huku akitoa
ahadi ya kutoa sh.milioni 5 kutoka mfuko wa jimbo kwa ajili ya kusaidia
ujenzi wa zahanati.
Post A Comment: