Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatoa hofu mashabiki wa Ommy Dimpoz kuhusu hali ya kiafya ya msanii huyo ambayo imezua taharuki kubwa.

Mwishoni mwa wiki iliyopita zilisambaa taarifa za hali ya Dimpoz kuwa mbaya na kukimbizwa hospitalini nchini Afrika Kusini.

Mhe. Makonda kupitia mtandao wa Instagram, ametoa taarifa kuwa hali ya msanii huyo inaendelea vizuri baada ya kuongea naye kwa njia ya simu.  

"Jana Saa 8 Usiku nilipata muda wa kuongea na rafiki yangu Ommy. Nilifurahi sana sana kupiga Stori na ndg yangu hasa kujua anaendelea vyema na soon tunarudi GYM @ommydimpoz," ameandika Mkuu wa Mkoa huyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: