Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amesema anashangazwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali na wasaidizi wao kuendelea kufuja fedha za halmashauri zao licha ya maneno mengi ya kukemea hali hiyo.

Akizungumza baada ya kuapishwa viongozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano Agosti Mosi, Mama Samia pia amewataka wakuu wa mikoa, makatibu tawala na makatibu wakuu kufanya kazi kwa kusimamia kiapo walichoapa na kuendeleza uhusiano mzuri kwa watakaowakuta maofisini mwao.

“Mnapokwenda huko mfanye kazi sambamba na ilani ya chama (Chama Cha Mapinduzi), hatutegemei tukizunguka hukio tukute mivutano.

“Halmashauri huko chini kuna mapato mengi ya kukusanywa lakini hayakusanywi ipasavyo na mengine yanakusanywa kinyume cha sheria.

“Mimi nashangazwa katika halmasahuri wakurugenzi na wasaidizi wao wanafuja fedha pamoja na yote tunayozungumza lakini bado huku chini kuna wanaume wanafuja fedha,” amesema Mama Samia.

Pamoja na mambo mengine, Mama Samia amewataka wakuu wa mikoa kusimamia na kutekeleza ilani ya CCM katika kutekeleza majukumu yao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: